
MWANZA: Mkuu wa Mkoa, CP Salum Hamduni amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalamu umeonyesha meli iko salama kufuatia kugonga Mwamba, na tayari wamewasiliana na Wizara ya Uchukuzi na Waziri mwenye dhamana kuhusu tukio hilo, huku hatua za kuunda timu ya uchunguzi wa kina zikiendelea. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) nalo limesema meli hiyo ilirejea salama katika Bandari ya Mwanza Kusini Saa 6:12 Mchana, na watu wote waliokuwemo melini walishuka salama na hakuna uchafuzi wa mazingira uliojitokeza. Katika hatua Nyingine, Rais Samia, akiwa Uganda, leo Novemba 18, 2026 amesema Tanzania inatarajia kuanza kwa safari za kibiashara za meli ya MV Mwanza kutoka Mwanza hadi Bandari ya Port Bell nchini Uganda, hatua inayolenga kuimarisha usafiri na biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki. Fuatilia zaidi jamii.app/MvMwanzaSalama #JamiiForums #Uwajibikaji #Utawala





















