←
Tanzania Media Women11,381 posts
Tanzania Media Women avatar

Tanzania Media Women

@TAMWA_

A peaceful Tanzanian society which respects human rights from a gender perspective. #ZuiaUkatili #WanawakeWanaweza

◷ Joined March 2013▧ 2,937 Photos and videos
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Nov 9

"Katika majadiliano ya namna bora za uzalishaji wa vipindi vya usawa wa kijinsia, bado watoa taarifa wamekuwa kikwazo hasa linapokuja suala la mimba na ndoa za utotoni hivyo mbinu zaidi zinahitajika kuwafikia wahusika na kupaza sauti zao," meneja wa Kituo, Niko Mwaibale,

Post attachment
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Nov 5

Mratibu wa Mradi wa Wanawake kwenye vyombo vya Habari/VIKES, Sylvia Daulinge amefanya ziara kwenye radio za kijamii ambazo zinaandaa vipindi vya usawa wa kijinsia kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na kuimarisha ushirikiano kati ya TAMWA na radio hizo. #tamwa #vikes

Post attachmentPost attachment
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Oct 9

Naibu Katibu Mkuu @WizaraYaMaendeleoYaJamii, Wakili Amon Mpanju, amesema mchakato wa kufuta vifungu vya 13na 17 vya Sheria ya Ndoa ya 1971 vinavyoruhusu ndoa za watoto chini ya miaka 18 unaendelea, ili kuendana na Sheria ya Mtoto ya 2009na Katiba ya Tanzania#TokomezaNdoaZaUtotoni

Post attachment
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Oct 5

Leo Dunia inaadhimisha Siku ya Walimu Duniani, walimu ambao wamehusika katika kuondoa vikwazo vya kijinsia, na kufungua milango kwa kila mtoto bila kujali jinsia yake. Maadhimisho ya mwaka huu yanabebwa na kauli mbiu isemayo:Simama na Walimu! Heri ya Siku ya Walimu Duniani @CWT

Post attachment
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Sep 28

Leo, wadau wa CORI tunaungana na dunia kuadhimisha #iduai2026 – Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa (International Day for Universal Access to Information) Upatikanaji wa taarifa kwa wote ni msingi wa uwazi, uwajibikaji, ushiriki wa wananchi na maendeleo jumuishi.

Post attachment
Tanzania Media Women avatar
Tanzania Media Women@TAMWA_·Sep 9

TAMWA kwa ufadhili wa VIKES (Taasisi ya Maendeleo ya Vyombo vya Habari - Finland) wamewakutanisha washirika wa mradi wa usawa wa Wanawake wanahabari (WIM) kutoka Uganda, Uganda Media Womens' Association(UMWA) na MCT kujadili hali ya usawa wa wanawake wanahabari Afrika.

Post attachmentPost attachmentPost attachment
Holy avatar
⟳ Tanzania Media Women retweeted
Holy@yose_hoza·Sep 4

Vyombo vya habari vinapaswa kuwa na sera nzuri zinazowalinda waandishi wanawake dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo rushwa ya ngono, vitisho vinavyoshusha uwezo wao wa kiutendaji. #womeninmediatz

Post attachment
Sonnino⚡ avatar
⟳ Tanzania Media Women retweeted
Sonnino⚡@sonnino123·Sep 7

🎙️ Sauti ya mwanamke ni muhimu sana katika tasnia ya habari Tunapaswa kuendelea na kuwa na sera za jinsia zinazohakikisha usawa, zinazoondoa ubaguzi na kutengeneza mazingira salama na jumuishi kwa wanawake katika vyombo vya habari. #womeninmediatz @TAMWA_

Post attachment
Mbundi John avatar
⟳ Tanzania Media Women retweeted
Mbundi John@JohnMbundi·Sep 7

Mifumo imara ya kiserikali na kisekta ni ngao muhimu katika kulinda wanahabari wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia. Inajenga mazingira salama kazini na inatoa msaada wa kisheria na kuvunja ukimya ili kulinda haki na usalama wao wa kiutendaji. @TAMWA_ #womeninmediatz

Post attachment