←
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿366,115 posts
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 avatar

𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿

@_zack255

Simba SC&Liverpool Fan | Mkulima | Alhamdulillah

◷ Joined June 2019▧ 50,632 Photos and videos
POOJA!!! avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
POOJA!!!@PoojaMedia·12h

In Tanzania before the game, the players supported by supporters club sang the National Anthem with their mouths cos there was no lights in the stadium as Tanzania NT did the same thing. They couldn't water the pitch of lack of electricity & none of their journalists that I followed mentioned it. But my country, it will be the contents for days. Again, Package Your Country ❤️

Kipanga avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Kipanga@Kipanga1986·5h

Ila Heche! Haya bana

Post attachmentPost attachment
chimbolavijana avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
chimbolavijana@chimbolavijana·5h

Ongeza hapo @maximudancer kwenye orodha ya Burudani🔥🔥 Eeh bwana eeh, hii ni kubwa sana 🔥🔥🔥 Unapataje nguvu ya kubaki nyumbani?? Hiyo tarehe 21 itakuwa ya 🔥🔥 sana 😁🙌🏼 #chimbolavijana #katoro #geita #fyp

Post attachment
Rashda Zunde avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Rashda Zunde@RashdaZunde·11h

UGANDA | NOVEMBA 18, 2026 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ameambatana na mmoja wa wanachama wa chama cha upinzani ili kujionea mwenyewe namna mambo yanavyoendelea na shughuli mbalimbali zinavyofanyika.

0:36
chimbolavijana avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
chimbolavijana@chimbolavijana·6h

Mwenyekiti kanyoosha maelezo, Jumba lote la sanaa linaamia Katoro katika Bata la Faida🔥🔥🔥 Huku tumechagua vibe na kuenjoy, ukikosa uwe na sababu ya msingi!!🙌🙌 #chimbolavijana #viral #tanzania #popular #geita

2:57
Afrika Jana na Leo avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Afrika Jana na Leo@AFRIKA_JANA·16h

Breaking Low birth rate is among the reasons this school has a shortage of students; only 79 pupils belong to this school, including the two finalists. @elonmusk has repeatedly asked people to produce as many children as they can to serve humanity 😄, and @MagufuliJP reminded people of this as well. According to the UN, Tanzania is among the countries with the highest birth rate, yet we find such a situation. So what’s happening in Japan, Hong Kong, etc.? What will it be in the next two decades?

Post attachment
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 avatar
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿@_zack255·7h

VIWANGO HOUSE (TBS) YAFIKIA ASILIMIA 95.2 YA UJENZI Ujenzi wa jengo la VIWANGO HOUSE la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) umefikia asilimia 95.2 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026. Jengo hilo litasogeza huduma za upimaji na uthibitishaji wa ubora wa bidhaa karibu na wafanyabiashara na viwanda vya Kanda ya Ziwa, kurahisisha shughuli za biashara na kuongeza fursa za upatikanaji wa masoko katika nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Post attachment
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 avatar
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿@_zack255·7h

DKT. MWIGULU AZINDUA KITAMBULISHO CHA TAIFA KILICHOBORESHWA ▪ Serikali yawekeza zaidi ya Sh. bilioni 30 katika kadi na mashine za uzalishaji ▪ Asisitiza wananchi kupata vitambulisho bila usumbufu ▪ Vitambulisho vya awali vinaendelea kutumika_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, akisisitiza kuwa uwekezaji huo unapaswa kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza usumbufu kwa wananchi. Katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mailimoja, Kibaha, mkoani Pwani, Waziri Mkuu pia amezindua teknolojia mpya ya uzalishaji wa vitambulisho, programu tumizi ya NIDA Wallet na magari 10 ya huduma za usajili. Amesema maboresho hayo yanafungua fursa ya kuunganisha huduma mbalimbali kupitia utambulisho mmoja, hivyo kupunguza ulazima wa wananchi kubeba vitambulisho vingi katika shughuli zao za kila siku. “Lengo la Serikali ni kuhakikisha uwekezaji huu unaleta matokeo yanayoonekana katika maisha ya kila siku ya Mtanzania,” amesema. Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa kila Mtanzania anayestahili kupata kitambulisho cha Taifa anapaswa kukipata kwa wakati, bila usumbufu wala urasimu. Amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha uwekezaji huo, akisema matumizi ya teknolojia yanapaswa kuboresha huduma, kuimarisha utawala bora na kupanua fursa za wananchi katika shughuli za kiuchumi. Akifafanua maboresho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji, amesema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 30 katika ununuzi wa kadi mpya na mashine tano za kisasa zenye uwezo wa pamoja wa kuzalisha vitambulisho 2,800 kwa saa. Amesema mashine hizo zinatumia teknolojia ya kuchora taarifa na picha kwa mionzi ya leza ndani ya tabaka za kadi, badala ya kuzichapisha kwa wino juu ya uso wake. Hatua hiyo inalenga kuongeza uimara wa kitambulisho na kupunguza uwezekano wa kughushi. Aidha, amesema nafasi za programu za kidijitali zinazoweza kuunganishwa kwenye kadi zimeongezwa kutoka nne hadi nane, ili kuwezesha matumizi mapana zaidi ya kitambulisho hicho katika huduma mbalimbali. Ameeleza kuwa uunganishaji wa huduma, zikiwemo bima ya afya, leseni za udereva na usafiri, utafanyika kwa hatua kulingana na utayari wa mifumo, makubaliano ya taasisi husika na matakwa ya kisheria. “Lengo si kuongeza teknolojia kwa ajili ya teknolojia, bali ni kumwezesha mwananchi kutumia utambulisho wake katika huduma mbalimbali kwa usalama na urahisi zaidi,” amesema Kaji. Kuhusu NIDA Wallet, amesema ni programu tumizi inayowezesha mwananchi kuwa na utambulisho wake wa kidijitali kwenye simu na kuutumia kuthibitisha taarifa zake wakati wa kupata huduma, kadiri mifumo ya taasisi husika itakavyounganishwa. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesisitiza kuwa uzinduzi huo hauondoi uhalali wa vitambulisho vya awali, hivyo wananchi hawalazimiki kubadilisha vitambulisho visivyo na dosari. “Hauna sababu ya kwenda kubadilisha kitambulisho chako cha zamani kwenda kupata kipya kama hakuna sababu yoyote ya msingi,” amesema. Katambi pia amewahimiza wananchi kuchukua vitambulisho vilivyo tayari katika maeneo walikojisajili. Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Paschal Inyasi Chinyele, amepongeza maboresho hayo, huku akisisitiza ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi, ushirikiano baina ya NIDA na taasisi nyingine na uendelevu wa teknolojia inayotumika.

Post attachmentPost attachmentPost attachmentPost attachment
Johari Mshana avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Johari Mshana@joharimshana·8h

Unaweza kushangaa unajitabilia nafasi bila kujua 😂! Mzee kila la kheriii. Wakuu wa wilaya member huyu 🏃

0:10
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 avatar
𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿@_zack255·7h

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Uganda uliongozwa na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu ya Entebbe, tarehe 18 Novemba, 2026.

Post attachmentPost attachmentPost attachmentPost attachment
Afrika Jana na Leo avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Afrika Jana na Leo@AFRIKA_JANA·11h

JOHN PAMBALU MBELE YA MAHAKAMA KUANZA KUVUNA MATOKEO YA UBISHI NA UJUAJI USIO NA TIJA Na Albert Pambalu, Magu Haya mambo yanaumiza sana, imagine ndugu yako anafanya vitu vya hovyo unamshauri lakini hasikii eti kisa kutafuta umaarufu wa kisiasa. Ukiwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na ukakosa busara unaweza kufikiria wewe uko juu ya sheria, shujaa na mtu asiyegusika hata na vyombo vya dola. Kiburi cha aina hii mwisho wake ni mbaya kwa kuwa unavunja sheria huku ukitoa maneno ya kishujaa. Kwa asiyefahamu mdogo wetu John aliamua kwa makusudi kuhamasisha vurugu zilizopelekea vifo vya watu wengi sana hapa Mwanza na maeneo mengine nchini na baadae aliamua kukimbilia nchini Kenya. Tupo tuliompa onyo mapema aache kufanya siasa zisizo na tija lakini hakuelewa. Leo hii anapandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kujitakia, nasema hivyo kwasababu baada ya kuhamasisha vurugu Mwezi October aliendelea hata ile Christmas aliwataka vijana watoke na kufanya vurugu japo wengi walimpuuza kutokana na somo la October. Yuko wapi Maria Sarungi aliyekuwa anakupa dola 600 kila Mwezi pale Nairobi? Je alikuonyesha yeye alipata kiasi gani kutoka Ford? Umetumika na sasa unakwenda kulipia. Vipi, kwani Kenya ulifukuzwa? Kwanini alikimbia na sasa amerudi? Sisi ndugu zako tulikupa ushauri uachane na siasa za kihuni lakini hukuelewa na ukaamini wewe ni maarufu kuliko shilingi sasa umetiwa nguvuni hujui kesho yako. Hii ni aibu kubwa kwetu! Anyways, mchuma janga hula na wa kwao. Wategemezi wako wote umetuachia sisi huku wewe ukiendelea kumtumikia shetani kwa siasa zinazohamasisha vurugu. Sote ni mashahidi namna ulivyotumia mdomo wako kuhamasisha vurugu Octoba mwaka jana, sasa ni wakati wa kupata mavuno yako. Fanya siasa lakini kamwe usivuke mipaka ya kutumika kuvuruga amani ya nchi yako. Tanzania ni moja tu na huu ni wito wangu hata kwa wale waliopo Canada ipo siku mtarudi na mtawajibika sawa sawa na maovu yenu "Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani". Karibu ngamani mdogo wangu Mwalimu John John Pambalu.

Post attachment
Samia Suluhu avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Samia Suluhu@SuluhuSamia·9h

Kwa vipindi tofauti, watendaji kutoka Tanzania na Uganda wamekuwa wakijadili utekelezaji wa makubaliano yetu. Leo, nikiwa katika ziara nchini Uganda, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni. Tumefarijika kuona hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa makubaliano hayo, hususan katika sekta za biashara, miundombinu, nishati na usafirishaji. Nimemweleza na kuikaribisha Uganda kuungana na Tanzania katika juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa meli, barabara, reli ya kisasa na usafiri wa anga, ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya kikanda na kimataifa. Aidha, nimempongeza Rais Museveni kwa hatua ya Uganda kuwa nchi ya kwanza kuanza ujenzi wa Ofisi za Ubalozi wake katika Mji wa Serikali wa Mtumba, jijini Dodoma, hatua inayotarajiwa kuhamasisha mataifa mengine kuwekeza katika eneo hilo.

Post attachmentPost attachmentPost attachmentPost attachment
Afrika Jana na Leo avatar
⟳ 𝐃𝐫.𝐙𝐚𝐜𝐤™🇹🇿 retweeted
Afrika Jana na Leo@AFRIKA_JANA·9h

Tanzania’s President allows opposition party members to observe her activities on foreign trips, promoting transparency, accountability, and inclusion in national affairs. Accompanying Her Excellency on foreign trips is a powerful gesture of unity and political maturity.

0:36